21 Agosti 2025 - 11:59
“Ushirikiano wa Kutekeleza Mpango wa Marekani na Israel” / Je, “Vita kama vya Karbala” vya Hezbollah Viko Mbele

Beirut – Baadhi ya wanasiasa na wabunge wa Lebanon wamewasilisha malalamiko rasmi dhidi ya Sheikh Naeem Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah, baada ya hotuba yake ya hivi karibuni aliyoituhumu serikali ya Lebanon kwa kutaka kuisalimisha nchi mikononi mwa Israel.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA, kikao cha malalamiko hayo kilifanyika Jumanne, tarehe 19 Agosti katika Ofisi ya Mbunge na Waziri wa zamani Ashraf Rifi katika eneo la al-Ashrafiyeh, Beirut.

Washiriki wa kikao hicho walijadili hotuba ya Sheikh Qassem, kisha kutoa taarifa rasmi wakiituhumu Hizbullah kwa kuchochea migawanyiko ya kidini na kuiweka nchi katika hatari ya vita vya ndani.

“Ushirikiano wa Kutekeleza Mpango wa Marekani na Israel” / Je, “Vita kama vya Karbala” vya Hezbollah Viko Mbele

Njama ya Kuondoa Silaha za Muqawama

Kwa mujibu wa uchambuzi wa Abdul Bari Atwan, mhariri wa gazeti la Rai al-Youm, mchakato huu si tu hatua ya kisiasa na kisheria dhidi ya Hizbullah, bali ni sehemu ya mpango mpana wa Marekani na Israel unaolenga kuanzisha vita vya ndani nchini Lebanon kabla ya kumalizika mwaka huu. Hatua hiyo inalenga kuhalalisha kisheria uamuzi wa Serikali, Urais na Bunge la Lebanon wa kuamuru jeshi kuivua Hizbullah silaha zake.

Atwan anabainisha kuwa silaha za Muqawama ni halali kwa mujibu wa Mkataba wa Taif, uliosisitiza kuwa ni lazima kuendelea kuzihifadhi kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi wa mara kwa mara wa Israel dhidi ya Lebanon.

Historia Inajirudia

Kwa mujibu wa wachambuzi, mzozo huu ni sawa na vita vya ndani vya kwanza vilivyoanza pia kutoka eneo la al-Ashrafiyeh, ambapo Lebanon ilishuhudia jitihada za kuivua harakati ya Palestina silaha zake. Tofauti ni kwamba, leo hii mashambulizi yanawalenga wapinzani wa Israel - Hizbullah, waliowahi kuishinda Israel mara mbili:

  1. Ukombozi wa kusini mwa Lebanon (2000).
  2. Kusimama imara katika vita vya Julai 2006.

“Vita vya Karbala” vya Hizbullah

Sheikh Qassem katika hotuba yake alisema wazi: Iwapo njama hii itaendelea, basi vita vya Karbala viko mbele yetuvita vya ushindi au shahada.”

Wanaharakati wa Muqawama wanasisitiza kuwa:

  • Silaha za Hizbullah hazijawahi kuelekezwa dhidi ya wananchi wa Lebanon.
  • Kila mara zimekuwa zikielekezwa kwa adui wa taifa – Israel.
  • Silaha hizo zinachukuliwa kuwa zimetakaswa na hutumika tu kwa malengo matukufu, hasa kulinda Lebanon na uhuru wake.

Kwa ujumla, Wanaotaka kuiondoa Hizbullah silaha na kuisukuma Lebanon kwenye vita vya ndani, wamepuuza ushindi wa kihistoria uliopatikana dhidi ya Israel na wanataka kurudia historia ya damu. Hata hivyo, wachambuzi wanaamini kuwa kama ilivyokuwa katika vita vya ndani vya awali, pia safari hii hawawezi kushinda – kwa sababu silaha za muqawama ni alama ya heshima, ulinzi na mshikamano wa kitaifa wa Lebanon.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha